Mwalimu wa Shule ya Msingi Mwanga, iliyopo Manispaa ya Kigoma Ujiji, Zakaria Richard amekamatwa na Jeshi la Polisi kwa madai ya kumbaka na kumlawiti mwanafunzi mwenye miaka 10, anayesoma darasa la tano katika Shule hiyo
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Kigoma, Kamanda wa Polisi Kigoma ACP. Martin Otieno, amesema Mwalimu huyo alikabidhiwa mtoto kwa ajili ya kumfundisha tuisheni ndipo akawa anatumia fursa hiyo kumfanyia ukatili.
"Tunamshikilia huyo mwalimu kwa kumfanyia vitendio vya kikatili, kwa sababu mwanzoni alikabidhiwa na wazazi wake lkini yeye akaenda mbali zaidi, na kumbaka na kumlawiti" amesema Kamanda Ottieno
Aidha RPC Otieno amewataka Wazazi kuwa na utaratibu wa kuwakagua Watoto na kuwapa nafasi ya kuwasikiliza pindi wanapokuwa na matatizo yao.