MUME wa Mtangazaji, Zamaradi Mketema, Shabani Hamisi leo Jumatatu, Novemba 4, 2019, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni akikabiliwa na kosa la kumtishia kumuua kwa kutumia bastola, Dereva wa lori la mchanga Venance John.



Shaban amefikishwa mahakamani hapo akitokea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kesi yake kushindwa kusajiliwa mahakamani hapo.



Mshtakiwa huyo amesomewa mashtaka yake na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mkunde Mshanga mbele ya Hakimu Mfawidhi, Frank Moshi, ambapo inadaiwa tukio hilo amelitenda Oktoba 30, mwaka huu maeneo ya Mbezi Mabwepande.