Msanii wa mashairi hapa nchini Mrisho Mpoto, ameieleza EATV & EA Radio Digital, kuwa katika maisha yake hajawahi kuamini katika ushirikina na kwenda kwa waganga, japokuwa suala lake la kutembea peku limekuwa likihusishwa sana imani potofu.

Licha ya watu kuhusisha suala lake la kutembea pekupeku na imani hizo, Mpoto amesema kuwa haamini katika ushirikina bali anaamini katika uhalisi wa kazi zake.

"Kamwe siamini katika hilo siamini kabisa kwa asilimia 100, wala sijawahi kutumia na sioni kama ina 'connection' yoyote, mimi naamini katika uhalisia na sidhani kama ushirikina unaweza kufanya kazi" amesema Mrisho Mpoto.

Aidha Mpoto ameongeza kuwa, "Nasikia na naona katika mitandao, mimi najizungumzia siamini katika ushirikina na huwezi kukuta nashiriki huko hata upepese, uchambue kwamba Mpoto aliwahi kupenya kwa mganga, akaambiwa ashike tunguli kamwe huwezi kukuta, mafanikio yangu yote kwenye 'game' naamini katika uhalisia ambayo inanifanya kunijenga kuwa msafi na kutanua wigo" ameongeza.