Urusi imeripoti kuwa mwanaume mmoja mjini Moscow anakabiliwa na kifungo cha miaka mitano au kutoa faini ya Euro 2400 sawa na shilingi za kitanzania milioni 6 kwa kosa la kumtishia polisi paka kama silaha yake na kumsababishia majeraha usoni na maumivu mwilini.

Mtuhumiwa huyo Gennady Shcherbakov mwenye umri wa miaka 59, anatuhumiwa kwa kumrushia polisi paka wakati ambapo polisi alikwenda kuthibiti kelele ambazo zilikuwa katika makazi ya watu zilizopigwa na jamaa huyo ambaye inasemekana kuwa amelewa.

”Alimshika paka huyo mabegani, na kumsababisha paka huyo kupatwa na hasira kali, akatoa makucha yake kisha kunirushia paka usoni mwangu” Amesema polisi huyo.

Malalamiko uchaguzi serikali za mitaa yatua TAKUKURU
Pia ameripoti kuwa kufutia tukio hilo limemsababishia kupata maumivu ya mwili, mikwaruzo katika pande za uso wake na kuwa amefanyiwa unyanyasaji kitu ambacho ni kosa la jinai.

Aidha, Kesi hiyo ilifunguliwa siku ya jumatano, ambapo ilikuwa ni kipindi cha zaidi ya mwaka tangu tukio hilo litokee , imeripotiwa

Kwa mujibu wa teevisheni ya taifa ya Urusi, tarehe 4 oktoba 2018, bwana Shcherbakov alikuwa amekuwa anapiga kelele katika makazi ya watu huko Moscow.