Aliyewahi kuwa Mrimbwende wa Taifa la Gambia mwaka 2014, Fatou Jallow amemtuhumu aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Yahya Jammeh kwa kumbaka na kumdharirisha.

Jallow ametoa tuhuma hizo mbele ya Tume ya Ukweli na Maridhiao na kusema kuwa Jammeh ambaye mwanzo alijifanya kama mzazi, akimpa zawadi na ushauri, alimlazimisha amkatae mchumba wake ambaye walipanga kuoana.

“Nimejaribu kuficha hii stori na kuufuta kichwani kwangu lakini imeshindikana, sikuopanda kuongea lakini nimeona ni wakati mwafka wa kusema, kile ambacho Rais jammeh alinifanyia ili Gambia na watu wengine wajue.

Yahya Jammeh aliikimbia nchi hiyo, Januari 2017 baada ya kushindwa katika Uchaguzi Mkuu na kukataa kutoka madarakani.

Mataifa ya Afrika Magharibi yaliingilia kati na Jammeh kutorokea Guinea Ya Ikweta ikiwa ni baada ya kukaa madarakani tangu mwaka 1994.