Mwanamke mmoja aliyekuwa maarufu duniani kwa kufuga nyoka na chatu, Laura Hurst (36) raia wa Indiana, Marekani, amekutwa ameuawa na chatu mwenye urefu wa futi 8.

Maofisa wa Polisi wamesema kuwa ndani ya nyumba yake wamekuta nyoka wengine 140.

Wameeleza kuwa walipigiwa simu ya dharula 911, majira ya usiku nakuelezwa  kuna mwanamke ambaye amevilingishwa na chatu wa futi nane shingoni katika eneo la Indiana.

Usiyoyajua juu ya ufugaji Ndevu
Mtaalamu wa afya alivyofika katika nyumba hiyo alimpima na kujaribu kumpa huduma ya kwanza lakini haikuzaa matunda, Laura alipoteza maisha.

Nyoka hao wamefugwa eneo maalumu ambao jumla wapo 140 huku marehemu Laura alikuwa anamiliki nyuka 20 na waliobaki ni wa mwenzake.