Mwanamitindo wa mavazi na urembo hapa nchini, Maza Sinare maarufu kwa jina la Maznat, ameeleza kuwa idadi kubwa ya wanaume siku hizi, wanawakimbia wanawake ambao wanatumia gharama kubwa kwenye kujiremba na kuwaasa wanawake kubaki na urembo wao wa asili.


Maznat ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye kipindi cha MAMAMIA, cha East Africa Radio, kinachoruka kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa, kuanzia saa 4 kamili hadi saa 6 kamili mchana.

"Kuna mtu ananunua wigi la laki 9, kuna wanaume wanaamua kukimbia kwa sababu ya hizo gharama, kila kitu nawasihi tufanye kwa kiasi, kwa sababu unaweza ukawa na muonekano wa asili na ukawa mzuri sana tu."amesema Maznat.

Aidha Maznat ameongeza kuwa, "Wanaume anajifanya wanapenda wanawake wanaovaa urembo sijui makalio makubwa lakini kamuangalir mtu  anayekwenda kumuoa wengi wao wako uzuri wao wa asili".

Maznat amewataka wanawake kujiamini na kujikubali wenyewe, kutokana na maumbile yao na kwamba wakijikubali wataweza kupata wanaume wenye vigezo sawa na vyao.