Mbunifu wa mavazi Tanzania na mshindi wa Tuzo nne za Afrika katika upande wa mavazi na uwanamitindo Martin Kadinda, amesema msanii Vanessa Mdee ni aina ya Mwanamke ambaye ni hadhi yake na anaweza ku-date naye.


Kutokea kushoto pichani ni Martin Kadinda kulia ni Vanessa Mdee.

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital katika uzinduzi wa "Reality Show" ya Irene Uwoya, Martin Kadinda amesema ukimuangalia Vanessa Mdee unaongelea  Mwanamke ambaye anaweza kuwa naye.

"Vanessa ni aina ya mwanamke ambaye ninaweza nika-date naye, nadhani huko ndipo nitaenda kuishia maisha yangu, ukimuangalia Vanessa unamuona mwanamke ambaye Martin Kadinda anaweza kuwa naye katika mahusiano" ameeleza Martin.

"Ila kwa sasa siwezi nikamtongoza kwasababu ni shemeji yangu na alikuwa na mahusiano na rafiki yangu Jux sina ustaarabu wa hivyo. Namuheshimu mtu ambaye anatoka na rafiki yangu na sijawahi kufanya hivyo', ameongeza.