Meja Jenarali Mstaafu Hamisi Semfuko akikagua gwaride la wahitimu wa mafunzo ya Jeshi Usu.
Baadhi ya wahitimu wakionyesha mbinu mojawapo ya kukabiliana na adui bila silaha
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Katavi wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi katika mafunzo hayo Meja Jenerali Mstaafu Hamisi Semfuko.
Mwenyekiti wa bodi ya mamlaka ya Uhifadhi Wanyama Pori Nchini (TAWA) Meja Jenerali Mstaafu Hamisi Semfuko amesema mfumo wa mafunzo ya Jeshi Usu yanayobadili watumishi wa Wizara ya Mali asili kutoka katika hali ya uraia wa kawaida na kuwa askari yameleta mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake miaka minne iliyopita
Amesema hayo wakati akifunga mafunzo hayo kwa wahitimu 535 katika Kituo cha Mafunzo Mlele mkoani Katavi.
Aidha amewataka wahitimu hao kuishi yale waliyojifunza chuoni hapokwa kipindi cha miezi mitatu katika kuhakikisha Tanzania inatokomeza kabisa matukio ya ujangili yanayofanyika katika hifadhi na mapori mbalimbali hapa nchini
Kwa upande wao baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo wameyasifu kwa kuwajengea ukakamau na kuwapa mbinumbalimbali za namna ya kukabiliana na adui
“Mbali na taaluma yangu ya uuguzi hapa nimeongezewa ujuzi ambapo sasa ninaweza kujumuika na askari katika doria na nikafanya nao kazi vizuri” alisema Ester Myaho ambaye ni mtumishi kutoka Wizara ya Mali Asili na Utalii
Pia wameiomba serikali kuboresha mazingira ya chuo hicho kwani kinakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo ukosefu wa jiko la kupikia chakula cha wanafunzi na bwalo la chakula pamoja na ukosefu mitandao ya simu za mkononi
Wahitimu hao wamepata mafunzo kadhaa ikiwemo namna ya kutumia silaha na kareti
Awali akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Katavi, Mkuu wa wilaya ya Mpanda Lililan Matinga alisema mkoa wa Katavi unashirikiana na Wizara ya Mali Asili na Utalii katika kulinda mali asili