MKUU wa wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga January Lugangika amesema kwamba wilaya hiyo wanahitaji nakala 3000 ya kitabu kilichoandikiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamini Mkapa kutokana na kwamba uwepo wa maeneo mengi ya kuuzia vitabu hivyo.

Kitabu hicho ambacho kimeandikiwa na Rais Mstaafu huyo ni cha “My Life, My Purpose (Maisha Yangu, Kusudi Langu)” ambacho kilizinduliwa Jumanne iliyopita na Rais Dkt John Magufuli.

Akizungumza na mtandao huu DC January alimpongeza Rais huyo mstaafu kwa kuamua kuandika kitabu hicho huku akieleza kwamba kwenye wilaya hiyo kuna maeneo mengi ya kuuzia kitabu hicho ikiwemo hoteli za kitalii na kwenye makazi yake

“Kwanza nimpongeze Rais awamu ya tatu Mstaafu Benjamini Mkapa hapa Lushoto ana makazi yake pia ni sehemu ya utalii anampongeza kwa kuandika kitambu ambacho kitakuwa ni hazina kubwa sana kwa kuwa watanzania hapa kwetu sisi tunapokea watalii wengi”Alisema

“Kwa mwaka 2018 tulipokea watalii 1400 na mwaka huu 2019 mpaka sasa tumepokea watalii 3000 na mtalii anapokuja Lushoto awe na kumbukumbu nzuri ni vizuri akanunua kitabu cha Rais Mstaafu Benjamini Mkapa kwa ajili ya kumbukumbu”Alisema.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba kumbumbuku nzuri hiyo ya kitabu mtu anaweza kuwa na kitabu anapotembelea makazi yake akikisoma anaweza kumuuliza swali lolote lile kuhusu kusudio la kuandika kitu ambacho amekiandika kwenye kitabu hicho.

Aidha alisema pia watajitahidi kila mwana Lushoto awe na nakala moja ya kitabu kuanzia maofisini, watumishi wa umma wote na sekta binafsi ili kuhakikisha kila mkazi wa wilaya hiyo anafuatilia maisha ya kiongozi huyo

“Lakini pia tutajitahidi kuongeza na watu wa vitabu wapate wakala mmoja na nisema sisi Lushoto tunahitaji si chini ya nakala 3000 tutaviuza kwa wakati”Alisema

Hata hivyo aliwataka watanzania waone umuhimu wa kununua vitabu vinavyoandikwa na viongozi wastaafu hasa ambao bado wapo duniani ni rahisi kuvisoma na kumpigia kumuuliza alipoandika jambo Fulani alikuwa na maana gani ni sehemu ya utalii na kumbukumbu.

“Lakini pia niseme tu kwamba Mkapa ni Lushoto na lushoto ni Mkapa hivyo sasa tupo tayari kusoma maisha ya kiongozi huyo kupitia kitabu chake na ndio maana tunahitaji nakala hizo “Alisema DC.