Mchekeshaji na muigizaji Idris Sultan, amesema kuwa ni vyema zaidi kama yataanzishwa mashindano ya kuvuana mawigi hii ni baada ya tifu alilolifanya Ebitoke siku za hivi karibuni la kumvua wigi mwanamke mwenzake katikati ya mkutano wa waandishi wa habari.

Idris amesema hayo kwenye mahojiano na EATV & EA Radio Digital, na kuwataka wanaume kuwa makini na wanawake zao

"Inapofikia wakati mwanamke anakurupuka na anakuja kuchomoa wigi la mtu mwingine kwenye mkutano ila kwangu mimi navyofikiria natamani sana kungekuwa na mdhamini wa wigi, kama ile 'show' ingekuwa tangazo hivi mtu anakwapua wigi na anakimbia nalo" amesema Idris Sultan.

Aidha Idris Sultan ameendelea kusema kuwa "Sina maelezo yoyote kutokana na jambo lile kusema ukweli, watu walifanya mambo yao ya faragha wanajua kabisa kimetokea nini, nawaambia tu wanaume waangalie na wajue mambo gani ambayo mnawapa wanawake zenu wasije wakacharuka kwenye 'press' wakati mnazindua vitu vyenu" ameongeza.