Mwinyi zahera akihojiwa na EFM leo mda mfupi uliopita akieleza mgogoro wa kufukuzwa umetokana na yeye kukataa kuchaguliwa kocha Msaidizi kwani hakumtaka Mkwasa na aliomba amchague msaidizi wake yeye mwenyewe lakini hilo limekua gumu kwa uongozi wake hali iliyopelekea kufukuzwa.

Vilevile Zahera ameeleza kuwa mashabiki wa Yanga wanadhani timu yao ina hela kwa sasa bila kutambua kilichopo nyuma ya pazia na akaamua kufunguka wazi juu ya hali halisi.

Akisimulia safari ya Gaborone Kuelekea mchezo dhidi ya Township Rollers Zahera anadai timu ilishindwa kukodi Bus la kuwapeleka wachezaji kutoka Johannesburg mpaka Botswana ambapo licha ya viongozi kufika siku mbili kabla lakini walishindwa kushughulikia hilo hali iliyopelekea kufuatwa na Bus la timu pinzani kitu ambacho si cha kawaida kutokea ulimwenguni.

Zahera anaeleza hali hiyo iliwachukiza Wachezaji wake kuwa haijawahi kutokea na walipofika Hotelini aliwaeleza viongozi nao wakajibu timu haina Pesa hivyo kufikia hatua ya kujitolea Kias cha Dollar 2000sawa na Tsh. Milioni 4 siku ya pili yake kwajili ya kukodi Bus litakalowapeleka mazoezini.

Wakiwa njiani kuelekea Gaborone wachezaji walikuwa wakihisi njaa viongozi wakasema hawana chochote Hali iliyopelekea Zahera kuwalipia Wachezaji Wote Chakula kitu kilichomfanya mmoja wa Kiongozi wa TFF aliyesindikiza msafara kumnong'oneza mmoja wa Wachezaji kuwa Mna bahati ya kupata Kocha.

Zahera anaeleza kuwa aliendelea kulipa hela Zake hata walipofika jijini Ndola Zambia aliendelea kuwalipia Gharama za Uwanja wa Mazoezi Dollar 200 kwa siku mbili huku akiendelea kulipia Chakula Wachezaji wake baada ya viongozi Kutaka kuwalisha wachezaji Mlo mmoja kwa siku wakiwa Zambia yaani wale saa 11 jioni tu bila chakula usiku(Pasi ndefu).

.....................MWANZA..................

Zahera anaendelea kusema kuwa Wakiwa Jijini Mwanza kujiandaa na mchezo dhidi ya #Pyramid_Fc Timu ilifikia katika hoteli ya hadhi ya chini huku huduma zake ikiwemo chakula kuwa za hali ya chini zaidi hali iliyopelekea kuomba namba ya Boss wa GSM kwa meneja Hafidhi na kumpigia Simu kumueleza hali halisi na kuomba msaada na bila shaka Boss huyo alisaidia Timu kuhamishiwa hoteli nyingine na huduma zikaboreshwa.

Lakini baada ya mchezo huo wachezaji wakiwa ndani ya Gari pamoja na benchi la ufundi walizuiwa kuondoka kwa madai  timu ilikuwa ikidaiwa vinywaji kiasi cha Dollar 500 alipoombwa na Makamu Mwenyekiti Fredrick Mwakalebela.

.......................Kuhusu Usajili................

Zahera anaeleza Wachezaji aliowasajili  kwa mapendekezo yake ni sita tu wakiwemo Sadney,Balinya,Bigirimana,Sibomana,Kalengo na mwisho ni Molinga huku akiikopesha pesa Klabu kumsajili #Faroukh_Shikalo.

...........Kuingiliwa Majukumu.........

Zahera anaweka wazi kuwa ilikuwa ni bora kufanya kazi na uongozi uliopita kwakuwa ulikuwa hauingilii majukumu yake ya kiufundi tofauti na uongozi wa mwenyekiti Mshindo Msollah kuwa kwakuwa ana taaluma ya ukocha amekuwa akiwachanganya wachezaji kwa kuwapa mbinu zilizo nje ya anayofundisha huku akitolea mfano mechi dhidi ya Lipuli Iringa walipopoteza kwa magoli mawili mwenyekiti aliingia vyumbani na kuanza kuelekeza mbinu tofauti na alizofundisha hali iliyopelekea Wachezaji kuulizana.

Kuhusu swala la Dante Zahera anadai Dante yuko sahihi kwani kabla ya kwenda AFCON aliuambia uongozi kuhakikisha unamalizana na wachezaji waliopo kabla ya kuleta wengine hivyo Dante angekuwa na kosa angemfanyia kama alivyofanya kwa Kakolanya.

#Source EFM_Redio na kuandikwa na 
#Mathiboy