Serikali ya Afghanistan imemuachia kiongozi wa kundi la Taliban Anas Haqqani na wafuasi wengine wawili wa kundi hilo baada ya makubaliano ya kubadilishana mateka na kundi la Kigaidi la Taliban.
Kwa upande wa Kundi la Taliban limewaachia raia wa kigeni wawili waliotekwa katika jiji la Kabul Miaka mitatu iliyopita nje ya jengo la chuo kikuu cha Marekani jijini humo.
Raia wa kigeni mmoja toka Marekani na mwingine Uingereza walikuwa Maprofesa walimu wa chuo hicho walitambuliwa kwa majina ya Kevin King Mmarekani na Timothy Weeks toka Australia Marekani.