GIGY Money siyo wa mchezomchezo, wakati Insta yote ikiamini kwamba yeye na Amber Lulu ni mashoga, juzi amemgeuka rafi ki yake huyo na kumtupia madongo kama yote. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Gigy alitangaza kupata rafiki mpya aliyemtaja kwa jina la She_queen kisha kumpa madongo Amber Lulu kuwa hakuwa rafi ki mzuri kwake.

“Majiraniii amkeni nimempata rafi ki mwenye akili timamu, sio mlevi halafu ana hela anaitwa She_queen,” aliandika Gigy Money bila kumtaja Amber, lakini wananzengo wanajua kwamba shosti yake mkubwa ambaye ni mpiga mitungi ni Amber Lulu, hivyo wakaambatanisha na picha yake kwenye posti zao mbalimbali