Mgeni Rasmi wakati wa Mahafali ya 11 ya kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom,Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi akikata utepe kwenye mahafali hayo.Aliyevaa nguo nyeusi nyuma ni Mkurugenzi wa shule ya Sekondari Kom, Jackton Koyi. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mgeni Rasmi wakati wa Mahafali ya 11 ya kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom,Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi  akiwasalimia wazazi na wageni waalikwa kwa kuwapungia mkono.
Wahitimu wa kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom wakiwa katika maandamano kuingia ukumbini wakati wa sherehe za mahafali ya 11 kidato cha nne mwaka 2019 shule ya Sekondari Kom ‘ Kom Secondary’ iliyopo katika eneo la Butengwa katika manispaa ya Shinyanga. Jumla ya wanafunzi 189 wamehitimu elimu ya kidato cha nne katika shule hiyo.
Wahitimu wa kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom wakiwa katika maandamano kuingia ukumbini.
Mgeni Rasmi Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi  akizungumza wakati wa Mahafali ya 11 ya kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom, ambapo alitumia fursa hiyo kuipongeza shule ya Sekondari Kom kwa mwenendo mzuri kitaaluma kwani imekuwa ikifanya vizuri kwenye mitihani mbalimbali.
Mkurugenzi wa shule ya Sekondari Kom, Jackton Koyi akitoa neno la salamu wakati wa Mahafali ya 11 kidato cha nne shule ya Sekondari Kom.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Kom, Mwita Waryoba akisoma historia ya shule ya Sekondari Kom. Warioba aliwaomba wazazi kuwaongoza na kuwaelekeza vizuri vijana waliomaliza elimu ya kidato cha nne wakati wakisubiri matokeo yao yatakayowawezesha kuendelea na masomo yao ya kidato cha tano na vyuo.
Wahitimu wa kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom wakikata keki maalumu wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019.
Wahitimu wa kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom wakikabidhi zawadi ya keki kwa walimu wa shule ya sekondari Kom.
Wahitimu wa kidato cha nne 2019 shule ya Sekondari Kom wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019.
Wazazi na wageni mbalimbali wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019.
Wageni waalikwa wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019 shule ya Sekondari Kom.
Wazazi na wageni mbalimbali wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019.
Wazazi na wageni mbalimbali wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019.
Onesho la mitindo ya ubunifu wa mavazi likiendelea.. Pichani ni vijana wakionesha ubunifu wa mavazi ya Mama Afrika wakati wa Mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019 shule ya Sekondari Kom.
Onesho la vazi mavazi ya wahudumu wa kwenye Ndege likiendelea wakati wa Mahafali ya 11 ya kidato cha nne mwaka 2019 shule ya Sekondari Kom.
Vijana wa Skauti wakionesha michezo ya ukakamavu wakati wa mahafali ya 11 ya kidato cha nne Kom Sekondari mwaka 2019.
Mgeni Rasmi Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi  akizungumza wakati wa Harambee kufanikisha ununuzi wa vifaa vya maabara katika shule ya sekondari Kom,ambapo makadirio ya gharama ya ununuzi wa vifaa hivyo ni milioni 6.
 Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi akichangia pesa wakati wa Harambee kufanikisha ununuzi wa vifaa vya maabara katika shule ya sekondari Kom.
 Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi akimpa Kampani ya kucheza mzee aliyejitokeza kuchangia pesa huku akicheza muziki wakati wa Harambee kufanikisha ununuzi wa vifaa vya maabara katika shule ya sekondari Kom.
Ukawadia muda wa kugawa vyeti kwa wahitimu wa kidato cha nne 2019 katika shule ya Sekondari Kom.
Zoezi la kugawa vyeti vya kuhitimu kidato cha nne likiendelea.
Zoezi la kugawa vyeti vya kuhitimu kidato cha nne likiendelea.
Walimu  wa shule ya sekondari Kom wakikabidhi zawadi kwa Mgeni rasmi ,Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga,Mohammed Kahundi.
Mshereheshaji 'MC' wakati wa mahafali akiendelea kutoa utaratibu wakati wa mahafali hayo.
Wazazi wakifurahia na kijana wao. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog