MKUU wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo ameeleza kuwa anapenda kutumia baiskeli kwa misele midogomidogo kwani ina faida mwilini mwake.

Akizungumza na Amani, Jokate alisema mazoezi ni kawaida yake ya kila siku hasa nyakati za asubuhi na yanamfanya kujisikia vizuri sana na kumfanya kuwa mrembo siku hadi siku kwani hazeeki kabisa.

“Kwa kweli mazoezi ni sehemu mojawapo ya maisha yangu ya kila siku na pia napenda sana kutumia baiskeli kama naenda sehemu ambayo siyo mbali au ofisini, halafu huwezi amini yananifanya nionekane mrembo na nisizeeke kabisa,” alisema Jokate ambaye ni mmoja wa wakuu wa wilaya wenye mvuto wa aina yake.