Leo November 18, 2019 Mbunge wa Bumbuli January Makamba pamoja na Wanakikundi wenzake wa kikundi cha RG Brothers wamefika anapoishi Mtoto Anna Zambi.

Akiongea na AyoTV January amesema “Pole kwa wafiwa na Mdogo wetu, kama unavyojua msiba huu umegusa taifa, umemgusa kila Mtu, kitu kikubwa kwenye msiba kama huu ni faraja”

Baba na Mama wa Anna pamoja na Ndugu zake watatu walifariki kwenye ajali ya gari wakati wakisafiri kutoka Dar kwenda Kilimanjaro kwenye graduation yake lakini Anna hakuambiwa mpaka alipomaliza Mitihani yake ya kidato cha nne.