Iran imetangaza leo hatua zake mpya za kukiuka makubaliano makubwa ya silaha za nyuklia yaliyosainiwa mwaka 2015 kati ya mataifa yenye nguvu kubwa duniani.

Iran imesema kwa sasa inatumia nyenzo ambayo ina kasi ya mara 50 zaidi ya ile iliyokubaliwa na mkataba huo.

Tangazo hilo limetolewa wakati Iran ikianzisha maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 40, tangu Marekani ilipoukamata ubalozi wake mnamo mwaka 1979, mzozo uliodumu kwa siku 444.

Mkuu wa shirika la kitaifa la nishati ya Atomiki nchini Iran Ali Akbar Salehi amesema kwa kuanza kutumia nyenzo hizo za kasi kubwa, Iran itapunguza muda wa mwaka mmoja ambao wataalam walisema Iran itauhitaji ili kuwa na vifaa vyote vya kutengeneza silaha za nyuklia endapo itaamua kufanya hivyo.

Iran ilishakiuka makubaliano hayo kuhusu urutubishaji madini ya urani kama hatua ya kuushinikiza Umoja wa Ulaya kupata mkataba mpya, mwaka mmoja tangu Marekani ilipojiondoa katika mkataba huo