Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Juliana Shonza anatarajia kuwa mgeni rasmi katika maonesho ya Red Ribbon Fashion Gala 2019 yatakayofanyika Novemba 30 mwaka huu katika Ukumbi wa Serena Hotel Jijini Dar es Salaam.
Maonesho hayo yameandaliwa na Ujuzi Initiatives chini ya Designer Nguli Khadija Mwanamboka ambapo itafanyika Novemba 30 mwaka huu ikiwa ni kuadhimisha siku ya Ukimwi Duniani.
Wabunfiu mbalimbali 12 wakubwa kutoka nchini wanaungana kwa pamoja kupambana na maambukizi ya Ukimwi kwa kutumia Ubunifu wao wa Mavazi
Mbunifu wa mavazi ya Stara, Irada Mahadhi Mtonga " Irada Style" amesema kuwa kwa mwaka huu Jukwaa la Fashion show hawatapanda wanamitindo pekee bali litakuwa na mchanganyiko wa watu mashuhuri mbalimbali watakaovalia mavazi ya wabunifu hawa kama kuonesha ushirikiano wao wa mapambano dhidi ya Ukimwi
Amesema, maonesho ya mwaka huu yatahudhuriwa na watu mashuhuri na kwa upande wake amejipanga kuonesha ubunifu wake mpya wa mavazi yake ambayo yamekuwa yanapendwa sana na wakina dada na mama.
Irada amesema pia hawataangalia wabunifu wakubwa tu, hata wazoefu, wachanga na wale wanaoanza wataonesha mavazi yao ikiwa ni jitihada za kupambana kwa pamoja katika kutokomeza maambukizi ya Ukiwmi kwa kutumia ubunifu
Wabunifu wengine watakaoshiriki kwa mwaka huu ni Martin Kadinda,
Jamila. Asya Hamsin, Malika. Khadija Mwanamboka, Jojo the African, Kulwa Mkwandule, Katty Collection, Zamda, Abdul Mwene, Melanin, Lucky na Bijoux na wengineo.
Watu wamshuhuri watakohudhuria ni pamoja na Lady Jaydee, Angela Bondo, wabuidu Ally Remtullah na Mustafa Hassanali huku kiingilio kikiwa ni 120,000 kwa viti vya VIP na kawaida ikiwa 35,000.
Mbunifu wa mavazi ya Stara, Irada Mahadhi Mtonga