Msanii  Idris Sultan aliyehojiwa na polisi  jana Alhamisi Oktoba 31, 2019 kwa saa tano na kupekuliwa nyumbani kwake ameachiwa kwa dhamana usiku wa kuamkia leo.

Baada ya kuhojiwa, mchekeshaji huyo ambaye jana alitakiwa kuripoti polisi na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alikwenda na polisi nyumbani kwake.

Wakili wake, Benedict Ishabakaki amesema licha ya kwamba Msanii huyo ameachiwa kwa dhamana usiku, atatakiwa kuripoti tena Kituo cha Polisi leo saa mbili asubuhi ili Polisi waendelee na upelelezi wao.

Idris alitakiwa kwenda polisi baada ya kuweka picha yenye sura yake huku akiwa ameketi katika kiti chenye nembo ya Taifa.

Pia, Idris aliweka picha nyingine inayoonyesha sura ya Rais Magufuli akiwa amesimama huku amevaa suruali yenye mikanda inayoshikizwa mabegani