Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema itatoa hukumu dhidi ya Rais wa zamani wa TFF Jamal Malinzi na wenzake watatu December 05 mwaka huu.

Malinzi, Mwesigwa, Mwanga na Flora wanakabiliwa mashtaka 20 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha Dola za Kimarekani 173,335.

Hukumu hiyo ilipangwa kusomwa jana lakini Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi, alisema bado haijakamilika na kwamba itasomwa tarehe iliyopangwa.

Kesi hiyo imesikilizwa na Hakimu Mkazi Maira Kasonde lakini kwa sasa amehamishwa kituo cha kazi

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, alidai kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kusikiliza hukumu na upande wa Jamhuri ulikuwa tayari.

Hata hivyo, Hakimu Shaidi alisema hukumu ya kesi hiyo itasomwa Desemba 5, mwaka huu na washtakiwa wataendelea kukaa mahabusu.