Mwanamuziki Diamond Platnumz, akiwa na baadhi ya wasanii wa Watakaopafomu shoo ya Wasafi Festival katika viwanja vya Posta Kijitonyama, jijini Dar es salaam. Wasanii hao wamefanya ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali leo kuanzia katika ofisi za Star Times na maeneo mengine ya jiji la Dar es salaama na kumalizia kukagua steji ya kimataifa itakayotumika Jumamosi.