MKUU wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Rosemary Staki ametangaza vita mpya na majangili wanaoingia kwenye hifadhi na kuua wanyama kwamba hawatapata nafasi kutokana namna serikali ilivyojipanga kukabiliana nao huku akieleza watakaokamatwa watashughulikiwa kwa hatua kali za kisheria.

Pia amewataka wabadilishe biashara hiyo na sasa waanza kujikita kwenye kufanya ujenzi wa hoteli za kitalii ili waweze kujiingizia kipato badala ya kufikiria kuendelea kufanya vitendo vya ujangili kwenye hifadhi.

DC Staki aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna kama serikali walivyojipanga kuhakikisha wanapambana na vitendo vya ujangili vilivyopo kwenye maeneo yao ambapo alisema watu hao hawana nafasi kwenye wilaya hiyo.

“Labda tu niwaambie kwamba hifadhi zote zina askari nikihesabu majeshi yote niliyokuwa nayo hatutawapa nafasi kwani serikali wamejipanga na ukienda kwenye hifadhi zote ni askari kwa maana ya kuzuia watu wasiingie na kuuwa wanyama na kuharibu mazingira hivyo na ambao watasubutu kufanya hivyo tutawachukua hatua kali kama tukikuta mvua anadhamira mbaya na hifadhi zetu tumesimama imara tunataka vivutio hivyo vizazi vya sasa na na vijavyo vivikute”Alisema DC Staki.

Alisema kwamba kasi ya serikali ni kuhakikisha inafanya utalii unakuwa sehemu ya kiuungia mapato kwenye nchi hivyo wo hawawezi kufanya uzembe ambao utafanya vivutio hivyo kupunguza hadhi yake au kupunguza sifa yake ikiwemo wanyama na kuharibu mazingira.

Hata hivyo alisema kwamba hivi sasa wanafuatilia maeneo ambayo wanyama walikuwa wanapita waone kama maeneo hayo yameendeleza kiasi gani au hayaendelezwa kama hayajaendelezwa yaachwe wazi kusiwe na muingiliano kati ya shughuli za binadamu na wanyama ili kuona namna ya kufanya ili kuondoa hali hiyo.

Akizungumzia suala la wafugaji kuingia mifugo kwenye hifadhi hiyo Mkuu huyo wa wilaya anasema kwamba changamoto hiyo ilikuwa ni kubwa ilikuwa inawasumbua sana lakini miaka ya hivi karibuni kutokana na juhudi kubwa za kusimamia sheria na kutoa elimu kwa wafugaji mifugo idadi ya mifugo inayoingia ngombe na mbuzi wanaoingia kwenye hifadhi hiyo.