Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo katikati mwenyesuti nyeus akizungumza na Kamati zilizoundwa na wananchi kwa ajili ya kuratibu na kusimamia zoezi la urasimishaji makazi. Kushoto wapili ni Katibu Tawala Stella Msofe.
 Wajumbe wa kamati zilizoundwa na wananchi kwa ajili ya kuratibu na kusimamia zoezi la urasimishaji makazi.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo katikati mwenyesuti nyeusi akiwa na Askari polisi pamoja na wanajeshi waliokuwa katika kikao cha Kamati zilizoundwa na wananchi kwa ajili ya kuratibu na kusimamia zoezi la urasimishaji makazi. Watatu kulia ni Mkuu wa Idara ya Mipango miji Maduhu Kazi.
 Mkandarasi David Emanuel mwenyesuti nyeusi akiingia kwenye gari mara baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni , Mhe. Daniel Chongolo kumuagiza Kamanda wa Takukuru mkoa maalumu wa Kinondoni kumchunguza kulingana na tuhuma zinazomkabili.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo amemuagiza Kamanda wa Takukuru Mkoa maalumu wa Kinondoni kumchunguza Mkandarasi wa Savei anayesimamia urasimishaji makazi ya wananchi kanda ya Madale two, David Emanuel kutokana na tuhuma ya kudaiwa kuiba kiasi cha shilingi milioni 52 fedha zilizochangwa na wananchi.

Ameongeza kuwa milioni 52 zimelipwa pasipokufuata utaratibu kutokana na mkandarasi huyo kuwa sehemu ya waweka saini katika akaunti ya wananchi na kwamba alichokuwa anakifanya nikwenda mwenyewe benki na kuchukua fedha..

Mhe. Chongolo amefikia uamuzi huo leo (jana) katika kikao chake na Kamati zilizoundwa na wananchi kwa ajili ya kuratibu na kusimamia zoezi la urasimishaji pamoja na wakandarasi waliopewa jukumu la urasimishaji makazi ya wananchi katika Halmashauri hiyo.

Mhe. Chongolo ameeleza kuwa mkandarasi huyo alijilipa mwenyewe fedha hizo pasipokufuata utaratibu na kwamba kitendo hicho ni matumizi mabaya ya fedha za wananchi na kuagiza Takukuru Kinondoni kumchukulia hatua pindi atakapobainika ukweli dhidi ya tuhuma hizo.

Amefafanua kuwa katika kanda hiyo, viwanja zaidi ya 1800 vimerasimishwa na hivyo wananchi wamechanga kiasi cha shilingi zaidi ya milioni 70 na kwamba hadi sasa mkandarasi huyo ameshalipwa shilingi milioni 62 ambapo kati ya hizo milioni 12 ndio zilizolipwa kwa kufuata utaratibu.

“ Sasa ukiona hivi unajua kabisa kunachangamoto ya matumizi yasio yasihi ya fedha za wananchi,nimechukua hatua nimemkabidhi Kamanda wa Takukuru mkoa maalumu wa Kinondoni, wamemchukua wanakwenda kushugulikia kufanya uchunguzi na pale watakapobaini kunaukiukwaji watamchukulia hatua” amesema Mhe. Chongolo.

Nakuongeza kuwa” kulingana na changamoto ambayo tumeibaini leo kwenye mtaa mmoja, nimeagiza kitengo cha ukaguzi wa ndani kwenda kukagua akaunti zote za urasimishaji ndani ya Halmashauri yetu ,ili kujiridhisha na yale watakayo yabaini sisi watuletee ripoti ilituweze kuchukua hatua stahiki kwa wakati muafaka”.

Awali Mhe. Chongolo amesema kuwa katika mkutano huo wanapokea taarifa ya kila mkandarasi juu ya mwenendo na matumizi ya fedha zinazochangwa kutoka kwa wananchi ilikukamilisha zoezi husika la urasimishaji.

Amebainisha kuwa , katika mkutano huo amejifunza kuwepo na changamoto ya usimamizi wafedha za wananchi katika maeneo mengi yanayoendesha zoezi hilo ipo haja ya haraka katika kutatua changamoto hizo.