RAPA matata Bongo, Claudia Lubalo ‘Chemical’ amesema kuwa ahadi yake aliyojiwekea ya kujioa ipo palepale na anaweza kujioa hata mara kumi.
Akizungumza na Showbiz Xtra, Chemical alisema kuwa hakuna kitu kilicho na thamani kama kujioa na kujimiliki mwenyewe maana utajijali na kujiangalia zaidi mwenyewe na wala siyo jicho la mtu mwingine.
“Mimi bado nasimama na maamuzi yangu ya kujioa mwenyewe, yaani naweza kufanya hivyo mara kumi na wala nisihitaji mtu pembeni. Mimi mwenyewe kwanza mgumu, nani wa kuumiza mtima wangu? Hakuna kabisa, nitajioa mwenyewe,” alisema Chemical.