Boti mpya ya Kilimanjaro VII inayomilikiwa na Bakhresa Group chini ya Azam Marine na ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa hamu imewasili leo kutoka kiwandani Australia.

Boti hiyo itakayokuwa na huduma za kisasa zaidi hapa Tanzania, imefika Zanzibar ikiwa imebebwa juu ya meli maalum.

Kwa mujibu wa kampuni ya Azam Marine, boti hiyo inafanyiwa ukaguzi na kukamilisha taratibu nyingine za kimamlaka kabla ya kutangazwa muda wa kuanza huduma zake.