Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Ally Laay (katikati) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela (kulia) wakimpongeza Mjumbe wa Bodi ya Benki hiyo, Prof. Neema Mori kwa kupata wadhifa wa uProfesa, hivi karibuni.
Prof. Neema Mori ni mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB na ni mhadhiri mwandamizi katika Idara ya Fedha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Pia ni muasisi na mkurugenzi wa kampuni ya uwekezaji ya MTI iliyopo Tanzania na Norway. Pia ni mkurugenzi na muasisi wa Chuo cha Uongozi na Ujasiriamali (Institute of Management and Entrepreneurship Management (IMED). Amewahi pia kuwa Doctoral Research Fellow Chuo Kikuu cha Agder, Norway. Prof Mori ana Shahada ya Ubobevu (PHD) katika biashara za kimataifa (utawala wa makampuni na bodi za taasisi za fedha) kutoka chuo kikuu cha Agder Norway.
Benki ya CRDB inafuraha kwamba sera yake ya usawa kazini, inayowapa vipaumbele wanawake katika nyadhifa mbalimbali za uongozi na kuhakikisha wanashiriki kikamimlifu katika shughuli za maendeleo inatekelezwa na kuzaa matunda.