Meneja wa WCB, Babu Tale amefunguka kuzungumzia ishu ya baadhi ya wasanii wa label hiyo nyota zao kushindwa kung’aa.



Lebo hiyo ina wasanii watano, ambao ni Diamond, Rayvanny, Mbosso, Lavalava pamoja na Queen Darleen.

Katika mahojiano maalum na gazeti la Mwananchi, Babu Tale alikiri kwamba Lavalava pamoja na Queen Darleen ni wasanii ambao nyota zao zimeshindwa kung’ara na kueleza hatua walizochukua.

“Kwenye familia za kawaida wapo watoto wenye mafanikio na ambao hawana, hivyo hivyo kwa familia ya WCB kuna baadhi ya wasanii nyota zao zimeshindwa kung’ara” alisema Babu Tale

Aliongeza, “Hivyo sisi kama viongozi wa labo tunachokifanya ni kuwatengenezea mazingira mazuri ya kufanya kazi zao, kama kila mmoja kumuuacha na meneja wake linalobakia ni jukumu lao kuangalia namna gani wanajiongeza,”

“Kama mnavyoona,  hivi karibuni Lavalava aliachia wimbo wa ‘Tekenya’. Naona kaamua kuwatekenya  mashabiki, na Queen Darleen  inshallah naye hivi karibuni  ataachia kazi”

Meneja huyo amedai wao kama WCB wanatoa mazingira sawa kwa kila msanii ili kuhakikisha anafanya vizuri katika safari yake ya muziki.

Source: Mwananchi