IKIWA ni siku chache tangu kuugua ghafla na kupooza kwa Seth Bosco ambaye ni mdogo wa aliyekuwa nyota wa filamu Tanzania, Marehemu Steven Kanumba, majanga yameendelea kuikumba familia hiyo ambapo baba mzazi wa Kanumba, Mzee Charles Kanumba naye yupo hoi akiugua.Baba Kanumba ambaye yupo nyumbani kwake mkoani Shinyanga, anasumbuliwa na tatizo la kibofu lililosababisha afanyiwe upasuaji hivi karibuni.Kwa upande wake Seth , yeye bado yupo kitandani baada ya kufanyiwa upasuaji na kugundulika ana tatizo kwenye uti wa mgongo.