Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kutaka Soko Kuu jipya la Dodoma kuitwa soko la Ndugai. Hatimae Spika, Job Ndugai ameibuka na kumshukuru.



Spika Ndugai ametoa shukurani hizo wakati akihitimisha Bunge la vijana 2019 lililofanyika kwa  Kipindi cha wiki moja katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma. ambapo amesema kuwa amefarijika pia.

“Namshukuru Mheshimiwa Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuliita soko Kuu jipya la Dodoma (Soko la Ndugai) nimefarijika sana ,“ Alisema Ndugai.