Tanzania Sweetheart ambaye ni Mwigizaji wa Bongo Movie na Mlimbwende wa Miss Tanzania 2006 Wema Isaac Abraham Sepetu amesema ikitokea amefariki basi akazikwe huko Zanzibar karibu na kaburi la baba yake mzee Abraham Sepetu.

Ikumbukwe siku 3 zilizopita Mlimbwende huyo amezimia mara 4 kwa nyakati tofauti tofauti kutokana na tatizo la kupungua uzito sana.