Amber Lulu amieleza Friday Night Live ya EATV, kuwa wakati anaanza muziki watu wengi walikuwa wanamchukulia poa na kumdharau, ila hao hao ambao walikuwa wanamsema sasa hivi wamekuwa chawa na wanamuomba misaada.Akizungumzia mafanikio yake kwenye muziki ambayo yamebadilisha maisha yake kwa asilimia kubwa, amesema sasa hivi anaringa na anapokea simu nyingi sana kutoka kwa watu hadi anachoka.

"Vitu vingi sana vimebadilika kutokana na muziki kama 'lifestyle', muonekano, kuvimba, na wanaonichukia, pesa na kila kitu. Wakati naanza game watu walikuwa wananichukulia poa sana walikuwa wananiona kama 'kidemu' flani hivi mizinguo tu" ameeleza

Amber Lulu ameendeleza kusema watu hao ambao waliokuwa wanamsema sasa hivi wamegeuka na kumkubali kwa kumuomba misaada na kutambua nini anafanya na wengineo wamekuwa mashabiki zake na chawa. ameeleza.