Jamaa huyo kwa jina la Danzak ambaye ni rubani aliyeajiriwa na shirika moja la ndege nchi za kiarabu, aliwahi kuripotiwa kutaka kumuoa Wema ambapo imeelezwa alituma ndugu na marafiki kwenda familia ya Wema kueleza nia yake hiyo Ili mambo yakienda vizuri amuoe. Katika interview mpya na Globalpublishers Wema alipoulizwa kuhusu hilo amesema amekataa sababu jamaa hana sifa za kuwa mumewe

"Ni kweli nilimuona, ni kijana mzuri ambaye kweli inaonesha alikuwa na nia njema na mimi lakini kwa kweli binafsi sikuwa tayari kuolewa naye, Kwa kweli hajakidhi vigezo ambavyo mimi nahitaji kuviona kutoka kwa mwanaume ambaye anataka awe mume wangu.” Amesema Wema

Ingawa alienda kusomea urubani na kuajiriwa, lakini Ikumbukwe huyo Danzak ni msanii wa Bongofleva aliyewahi kuwa katika kundi la TNG Squared na kina Malick Bandawe aliyezaa na Rose Ndauka, sasa Wema alipoulizwa je jamaa kuwa msanii hadi sasa ni moja ya sababu ya kumkacha? Wema amejibu

“Nilivunjika sana moyo kwa kweli baada ya kuona tena ni msanii yaani sijui nisemeje lakini kwa kweli nilianza kuona kwamba hawezi kuwa siriazi, angekuwa na hiyo kazi ya urubani pekee ningejaribu kumfikiria mara mbili,” Wema ameiambia Globalpublishers

Pamoja na hayo ikumbukwe Pia kuwa hivi karibuni Wema ametamka kuwa hana mpango wa kuolewa kwani anaamini mambo yake mengi ya kimaendeleo yatakwama akiolewa na kuanza kumtumikia mwanaume. Hata hivyo, sweetheart huyo anasaka mtoto kwa udi uvumba