Mwalimu wa Chuo cha Ufugaji Nyuki cha International Beekeeping Open School & IPPE, Salvatory Millinga (wa pili kushoto) akiwaelekeza wanafunzi wa chuo hicho namna ya kulina asali kutoka kwenye mzinga wakiwa katika mavazi maalumu wakati wa mafunzo yaliyofanyika katika Kijiji cha Nyuki cha Kisaki mkoani Singida juzi.
 Rais wa Umoja wa Vijana Wajasiriamali na Wataalamu wa Miradi Mkoa wa Singida (SYECCOS) Philemon Kiemi akuzungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) waliotembelea Kijiji cha Nyuki cha Kisaki kilichopo nje kidogo ya Manispaa ya Singida.
 Kiwanda cha kuchakata asali kilichopo katika kijiji hicho cha nyuki.
 Mafundi wakichimba shimo la maji taka yanayotoka katika kiwanda hicho.
 Wafanyakazi wa kiwanda hicho wakipanga chupa zenye asali kabla ya kupelekwa sokoni.
 Rais wa Umoja wa Vijana  Wajasiriamali na Wataalamu wa Miradi Mkoa wa Singida (SYECCOS) Philemon Kiemi akiweka asali iliyochakatwa kwenye chupa ya nusu lita tayari kwa kuwekwa lebo na kupelekwa sokoni.
 Kiemi akiwaonesha waandishi mashine ya kuchakata asali jinsi inavyofanya kazi.
 Kiemi akizungumza na mmoja wa wanafunzi wanaosoma katika chuo cha ufugaji nyuki kilichopo kwenye kijiji hicho cha nyuki aliyetokea mkoani Ruvuma.
 Fundi mkuu wa kutengeneza mizinga ya nyuki akionesha moja ya mizinga ya kisasa ya nyuki ambayo inatengenezwa katika kijiji hicho.
 Moja ya bweni la kulala wanafunzi 12 linaloendelea kujengwa katika kijiji hicho cha nyuki.
 Mizinga ya nyuki ikiwa katika kijiji hicho cha nyuki.
 Baadhi ya magari yanayotoa huduma ya usafiri katika kijiji hicho.
 Jengo la ofisi kuu ya kijiji hicho likiendelea kujengwa.
 Kiemi akiwaonesha wanahabari shamba la kijiji hicho.
 Kiemi akionesha namna ya mizinga ya nyuki inavyotakiwa kuwekwa kwa mpangilio.
 Hapa Kiemi akitoka kukagua moja ya ofisi inayojengwa kwenye kijiji hicho.
 Mzinga ukiwa umening'inizwa kwenye mti.
 Madaraja ya reli ni moja ya kivutio cha utalii kwenye kijiji hicho cha nyuki.
 Muonekano wa jengo la Utawala katika kijiji hicho.
Wanafunzi na Mwalimu wa chuo cha ufugaji nyuki katika kijiji hicho  Salvatory Millinga (wa pili kushoto) wakionesha uvaaji wa vazi maalumu la kulinia asali.

Na Dotto Mwaibale, Singida.

WAFUGAJI wa nyuki nchini wametakiwa kuacha dhana ya kuelewa kuwa nyuki wanamazao mawili  tu za asali na nta wakati wanamengine matano yenye thamani kubwa.

Hayo yalisema juzi na Rais wa Umoja wa Vijana wa Wajasiriamali na Wataalamu wa Miradi Mkoa wa Singida (SYECCOS), Philemon Kiemi wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea Kijiji cha Nyuki cha Kisaki kilichopo nje kidogo ya Manispaa ya Singida.

" Pengine kutokana na uelewa mdogo wa wakufunzi wa ufugaji nyuki ndio uliosababisha wafugaji wa nyuki hapa nchini kubaki na dhana ya kuwa mazao ya asali na nta ndiyo yenye thamani kubwa katika ufugaji wa nyuki" alisema Kiemi.

Kiemi alisema nyuki wana mazao mengine matano ukiondoa nta na asali yaliyozoeleka na wananchi na wafugaji ambayo yanathamani ndogo sana.

Aliyataja mazao hayo mengine yatokayo na nyuki na bei zake kuwa ni Gundi ambayo bei yake kwa kilo ni sh.150,000, maziwa sh. milioni 4 kwa lita, chamvua sh.300, 000 kwa kilo,supu ya nyuki sh.50,000 kwa lita na sumu ya nyuki sh.400,000 kwa gramu.

Alisema mkulima aliyedhamiria kufuga nyuki kiukweli hawezi kutamani kufanya biashara nyingine kutokana na kipato kikubwa anachoweza kukipata ambapo hata akiuza gunia moja tu la mahindi haliwezi kufikia thamani ya kilo moja ya zao la gundi litokanalo na nyuki.

" Ufugaji nyuki hauhitaji madawa mvua wala gharama yoyote zaidi ya kuwa na mizinga yako lakini kilimo cha mahindi, alizeti na mazao mengine kinahitaji mahitaji mengi kama mbolea, madawa, mvua na mambo mengine yanayo mgharimu mkulima tofauti na ufugaji wa nyuki" alisema Kiemi.

Akifafanua zaidi Kiemi alisema ana ndoto ya kuwabadilisha asilimia 70 ya wakulima hapa nchini ili wawe wafugaji wa nyuki kwa sababu ufugaji wa nyuki unatunza mazingira, unatoa ajira nyingi na soko lake ni kubwa ndani na nje ya nchi akitolea mfano wa bei ya gunia moja la mahindi na mbuzi mmoja ni sawa na lita moja ya asali ya nyuki wadogo.

Kiemi ambaye ana vijiji  vitatu vya nyuki mkoani Singida vyote vikiwa na ekari 7000 ni mfugaji wa nyuki wa kwanza Barani Afrika kwa kuwa na mizinga zaidi ya 13,000 akizidiwa na raia mmoja wa Mexico aitwaye Miel Carlota ambaye wanakampuni ya watu watatu wenye mizinga makundi 50,000 na anamashamba 318 ambapo alisema mpaka ifikapo mwaka 2021 anataka kuwa na mizinga 20,000 na kuwa mfugaji wa nyuki namba moja duniani.