VIDEO: Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo amepiga hodi kwa Manny Pacquiao

VIDEO: Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo amepiga hodi kwa Manny Pacquiao

Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo ambaye hivi karibuni amejizolea umaarufu mkubwa kwa kumpiga bondia Sam Eggington wa England (September 28 2019) round ya pili kwa TKO katika pambano la round 10 nchini England na baadae kumpiga bondia wa Argentina Sergio Gonzalez pambano lililochezwa Nairobi Kenya (March 23 2019) kwa kumpiga kwa TKO round ya 5.
Sasa anajiandaa kupambana na bondia kutoka Philipines November 29 2019 uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam dhidi ya Arnel Tinampay ambaye anaonekana kuwa na CV nzito akiwa ni bondia namba moja kwa ubora Philipines wa uzito wa KG 69 lakini ni wapili katika taifa hilo kwa ubora baada ya Manny Pacquiao.
Kubwa walilokuwa wanahofu watanzania ni kuhusiana na Arnel Tinampay kuwa ni bondia anayetoka katika kambi ya Manny Pacquiao kitu ambacho Mwakinyo ameeleza kupitia AyoTV kuwa hakiwezi kumtisha kwani atampiga na Pacquiao atapata habari zake, Mwakinyo ni bondia namba moja kwa ubora Afrika na namba 19 kidunia katika uzito wake