RAPA The Game amekutwa na kisanga cha kulipa $7 millions, sawa na Tshs billion 16 baada ya kushindwa shauri lake linalomkabili la unyanyasaji wa kingono.
Mahakama nchini marekani imelitupilia mbali ombi la Rapper huyo la kusikilizwa upya kwa kesi hiyo na atatakiwa kulipa fedha hiyo kama ilivyo amuliwa.
Shitaka hilo lililofunguliwa 2015, na kati ya wanadada walioenda kwenye usahili wa Reality show ya The game iliyoitwa She’s got game bibie Rainey aliripoti kufanyiwa vitendo vya unyanyasaji baada ya Rapper huyo kumuita Rainey bar siku baada ya usahili.