ZIKIWA zimepita wiki chache tangu ajifungue, mtangazaji wa redio kutoka Mombasa, Kenya, Tanasha Donna Oketch amefungukia ujio wa albamu yake ya nyongeza (Extended Play –EP).Tanasha ambaye amezaa mtoto mmoja na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alisema EP yake hiyo ameipa jina la Donna Tell.Alisema EP hiyo itakuwa na mikwaju mitano na kuna mbili ambazo amezifanyia kolabo ambapo mojawapo amefanya na rapa kutoka nchini Nigeria, MI na nyingine bado hajamuweka wazi.“Majina ya ngoma kutoka kwenye EP yangu ni pamoja na Traitor, Gbedu (African Drum), Pour La Vie, This Love na Wine,” alisema Tanasha. Hata hivyo bado hajaweka wazi lin EP hiyo itadondoka.