Msanii wa Bongo Fleva ,Shilole amempongeza Waziri wa Maliasili na utalii, Hamis Kigwangala kwa kuanzisha kampeni ya Twenzetu Kileleni inayoshirikisha wasanii wa aina mbalimbali nchini kufanya utalii Mlima Kirimanjaro.

Wiki kadhaa zilizopita wasanii wa muziki na maigizo waliungana pamoja kufanya utalii wa ndani ambapo walikwenda kupanda Mlima Kilimajaro katika kuhamasisha utalii wa ndani.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram Shilole alisema ki kubwa alichovutiwa na kampeni hiyo ni kuona Waziri Kigwangala naye akijumuika na wasanii katika kufanya utalii huo na kwamba wengi watahamasika kwenye hilo.

"Mimi sikwenda, ila nimehamasika zaidi na nitak wenda lazima kama sio peke yangu nitakwenda mwakani ikija tena," alisema Shilole.

Alienda mbali zaidi na kumpongeza msaniiMwanaFA aliyewakilisha vyema utalii huo kwa kufika kilele cha Mlima Kilimanjaro pamoja na wasanii wengine akiwemo Nurdin Bilal

Aliwapongeza wote walioshiriki utalii huo na kwamba watahamasisha na wengine hata wasiokuwa wasanii katika kufanya utalii.