Mwanamuziki wa Bongofleva nchini Shilole, amefunguka na kusema kuwa moja ya wasanii ambao walimpa ahadi na hawakuitekeleza ni mkali wa BongoFleva Juma Jux, ambaye aliahidi kumlipia ada mtoto wake.


Shilole ametoa kauli hiyo katika kipindi cha Kikaangoni, kinachoruka kupitia kurasa za Facebook na YouTube ya East Africa TV, kuanzia saa 8 : 30 hadi saa 9 : 30 Mchana, ambapo amesema mpaka sasa hajalipa hiyo ada.

"Siku ya harusi yangu Jux aliahidi atamsomesha mtoto wangu mmoja, mpaka leo kaingia mitini, Jux naomba utimize ahadi yako lipa ada ya mtoto wangu ahadi ni deni" amesema Shilole.