Moja ya mijadala mingi iliyoko mitandaoni ni kuhusu Harmonize kujiondoa Kwenye lebo yake ya WCB,Ukifuatilia comment za mijadala hiyo wengi mashabiki wa Diamond platnumz (WCB) wanadai huo ndo mwisho wa Harmonize,in short atapotea kwenye game,Hilo hatuwez kubishana nalo coz ndo mfumo wa mziki wetu kuwa mikonon mwa baadhi ya watu.

Ila swali Langu ni je,WCB wana uwezo na nguvu tena ya kumtengeneza Harmonize mwingine?

Nakumbuka miaka kadhaa nyuma kuna lebo ilikuwa inajigamba kumtengeneza JAYZ na kumfikisha pale alipo,Siku moja Jayz akiwa anahojiwa na kituo kimoja aliulizwa kuhusu Hao watu wanao jigamba kumtengeneza yeye,Jayz aliwajibu "Kama ni rahisi kumtengeneza Jayz Basi wamtengeneze Jayz mwingine"

Swali Langu bado ni lile lile,Je WCB wanao uwezo tena wa kumtengeneza msanii wa levo ya Harmonize? Mana kwa wasanii walioko pale WCB hakuna wakufika Hata nusu ya Levo ya Harmonize ukimwondoa Diamond.

#Jimmy-The-Inimitable