MWANAMITINDO na mjasiriamali maarufu Bongo, Jane Rimoy ‘Sanchi’, amewakata vilimilimi baadhi ya watu wanaomfikiria baby wake anakuwa katika hali gani anapomuona ametupia picha za kihasara mitandaoni.

Sanchi ameliambia Gazeti la Ijumaa Wikienda kuwa, watu wanasema tu kwa sababu hawajua kwamba mpenzi wake ndiye anataka hivyo na kama yeye amepitisha hilo, nani apinge?

“Mpiga picha wangu ni baby wangu, watu wanaongea sana hawajui hilo, kama yeye ndivyo anavyotaka, hao wanaopinga wao ni nani?” Alihoji Sanchi anayesifika kwa picha za nusu utupu kwenye mitandao ya kijamii.