MWIMBAJI wa muziki wa Injili Bongo, Rose Muhando ameibuka na kuapa kuwa anawaburuza mahakamani wale wote wanaotumia jina lake na kumchafua.Kupitia msemaji wake, Daud Mashimo alisema, Rose anawashtaki wale watumishi wa Mungu wote wanaotumia jina lake kwenye matangazo ya mikutano au matamasha yao wakisema atakuwepo kutoa huduma ya uimbaji na mwisho haonekani kitu ambacho kinamchafulia jina na kuonekana anatapeli.“Rose atakaa na wakili wake, notice ya siku 14 itatoka Jumanne ijayo na baada ya hapo atawapeleka mahakamani baadhi ya watumishi ambao wamekuwa wakitangaza kuwa anakuwepo kwenye mikutano yao wakati hana taarifa nao na kumchafulia jina,” alisema Mashimo.