Malkia wa nyimbo za injili africa mashariki na kati mwana mama Rose Muhando week moja iliyopita aliweka wazi kuwa hana mtoto wake wa kumzaa ambaye anaimba

"Nina watoto watatu na katika watoto wangu hakuna mtoto wangu ambaye ameanza kuimba hapana japo mwanangu wa kwanza anapenda sana kuimba ila mpaka amalize shule kwanza na kama ni kuimba ataimba huko akisha maliza shule"

Aliongeza kwa kusema

" Nimesikia muda mrefu kuna watu wanaimba wanasema mimi ni mama yao mzazi hapana mimi sina mtoto ambaye ameanza kuimba"

Star huyo aliwataja watoto wake kwamba ni Gift, Nicolous na Millan na wote wapo shule