MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amewacharaza bakora wanafunzi 14 wa Shule ya Sekondari Kiwanja wilayani Chunya ambao wamekutwa na simu shuleni hapo. Wanafunzi hao wanahusishwa na tukio la kuchomwa moto mabweni mawili ya shule hiyo ambayo yaliteketezwa Septemba 30, 2019.