Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amekataa wito wa Marekani wa kusitisha mapigano kaskazini mwa Syria, akisema kuwa Uturuki itaendelea na mashambulizi yake.

Ameeleza hayo wakati ambao Naibu wa wa Marekani ,Mike Pence na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo wakiwa wanajiandaa kuja kufanya makubaliano.

Marekani yaiwekea vikwazo Uturuki kunani?
Siku ya jumanne, Urusi ilitoa angalizo kuwa haitaruhusu mapigano kutokea tena baina ya majeshi ya Uturuki na Syria.

Uturuki imesema kuwa lengo la kuendelea na mapigano hayo ni kutaka kuwaondoa wanajeshi wa kikurdi katika mipaka.

Uturuki inaaminika kuwa wanamgambo wa kikurdi 'Kurdish-led Syrian Democratic Forces (SDF)' ni asasi ya kigaidi .

Vikosi vya Uturuki pia vimebuni kile ambacho serikali yao inataja kuwa "eneo salama" la kuwapa makazi wakimbizi milioni mbili wa Syria ambao wamepewa hifadhi katika nchi hiyo.


Nini cha kufanya kama humpendi 'Bosi' wako?
Kujiondoa kwa majeshi ya Marekani katika ukanda huo kulitangazwa wiki iliyopita na kuipa Uturuki mwanya wa kuanza mashambulizi, mkosoaji wa serikai ya Trump alieleza.

Marekani ilirudia kukanusha hilo siku ya jumatatu.

Wananchi wengi wameuwawa katika oparesheni hiyo na watu wapatao 160,000 wamekimbia makazi yao, kwa mujibu wa UN.

Rais Erdogan amesema nini?

"Wanataka tuache kupigana '. Hatuwezi kusitisha mapigano hayo," bwana Erdogan aliwaambia waandishi siku ya jumanne.


" Wanatulazimisha kusitisha mapigano huku wakitangaza kutuwekea vikwazo.Lengo letu liko wazi kabisa.Hatuna hofu na vikwazo vyovyote," rais Erdogan aliongeza.