Rais John Magufuli amewaasa watoto wa kike kusoma na kusema ni aibu ya mkoa kuwa na idadi kubwa ya watoto waliopewa mimba na hali hiyo inasononesha wazazi na Serikali kwani Rukwa ni miongoni mwa mikoa iliyoongoza.

Aliyasema hayo jana wakati wa ziara yake ya siku tatu Mkoani Rukwa ambapo anafungua na kukagua miradi ya Maendeleo pamoja na kuzungumza na Wananchi wa Maeneo mbalimbali ya Rukwa na Wilaya zake

"Msubiri hata chungwa huwa haliliwi likiwa bichi, hata embe ambalo halijakomaa huwa chungu, ninyi bado ni wachungu," Rais Magufuli.

Aidha amewaomba wanafunzi hao kujiepusha na suala la ngono na kuwatahadharisha kuwa licha kupata mimba lakini pia yapo magonjwa hatarishi kama Ukimwi na kuwataka wamalize shule