Ndege mpya ya pili aina ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imeondoka nchini Marekani Oktoba 25, 2019 na inatarajia kutua jijini  Dar es Salaam, Tanzania leo Oktoba 26, 2019.

Ndege hiyo kubwa yenye uwezo wa kuchukua abiria 262 inatarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na kupokelewa na wananchi wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.


Hii inakuwa ndege ya 8 kati ya ndege 11 zilizonunuliwa na Serikali kwa lengo la kuimarisha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), kukuza utalii na uchumi.