EATV & EA Radio Digital, imepiga stori na msanii wa filamu Yusuph Mlela, ambaye amefunguka kuhusu mastaa kudanganya umri, pamoja na suala la Nay Wa Mitego kuwachana baadhi ya wasanii ambao wanatembea na mabaunsa.Yusuph Mlela amesema hayo baada ya kuweka wazi umri wake, wakati alipokuwa anafikisha miaka 33 ya kuzaliwa kwake siku ya Oktoba 10, 2019.

"Nafikisha miaka 33 kamili kwa sababu utu uzima ukiingia haupaswi,  muda ukishafika halafu ukishakuwa mtu mzima haina shida lazima useme ukweli", amesema Mlela.

Aidha akizungumzia kuhusu msanii Nay wa Mitego kuwachana wasanii ambao hawana hadhi na pesa ila wanatembea na ulinzi wa mabaunsa, Mlela amesema,

"Nay wa Mitego ni mtoto mdogo tu kwangu mimi, hajui anachokiongea yeye ni mtu wa kuongea ongea tu kwahiyo siwezi kumuongelea sana ila suala la usalama ni muhimu ukishafikia hatua fulani ya maisha lazima uwe na ulinzi, ambapo wataweza kukuangalia na kukuongoza ni mbuzi tu hata aki-diss sina wasiwasi naye"