Mrembo, Mfanyabiashara na Video Vixen Bongo Official Nai, amenyoosha maelezo kuwa kwa sasa hana bifu tena na Gigy Money, ila ameonekana kupata kigugumizi kumuongelea Amber Lulu ambaye amesema ni Mbulula.


Kupitia EATV & EA Radio Digital, Official Nai, amesema kwa sasa hana bifu na Gigy Money na wanataka kufanya kolabo kwani mwaka huu anaingia kwenye muziki ila hawezi kumuongelea mbulula ambaye ni Amber Lulu.

"Mwaka huu naingia kwenye muziki nina kolabo na Gigy Money , sikuwa na mipango yoyote na Amber Lulu na simuongelei mbulula, hatuwezi kumuongelea na kwanini tumuongelee yeye  na haina haja wala sababu ya kumuongelea " ameeleza Official Nai

Aidha amezungumzia kuhusu kutokuwa na tofauti na Gigy Money, baada ya kualikwa kwenye uzinduzi wa bidhaa fulani ambayo balozi mkuu ni Gigy Money amesema.

"Nimetokea hapa kwa sababu aliniambia kabla pia ni rafiki yangu na msichana mwenzangu tupo kwenye soko moja kupeana misaada ni kitu kizuri hata kama huko nyuma tulikuwa tinatofauti,  watu wengi hawakufikiria kama ninaweza kuwepo hapa hatuna tena tofauti wala bifu" ameongeza.