ALIYEWAHI kuwa kuwa bodygard wa msanii #DiamondPlatnumz, Mwarabu Fighter amempongeza Rapa wa Bongo, Nay wa Mitego baada kuongelea mabaunsa wanaowalinda wasanii wasiokuwa na vigezo vya kulindwa.Mwarabu Fighter amesema kuwa kitendo cha mabaunsa kuwalinda watu wasiopaswa kulindwa ni kuivunjia heshima tasnia ya ulinzi.


Mwarabu amesema hayo alipokuwa akizungumza kwenye kipindi cha #MidMorningFresh cha +255 Global Radio kinachorusha matangazo yake kutoka Sinza Mori Dar es salaam Tanzania.Amesema kuwa anapongeza Nay wa Mitego kutokana na kauli yake kwa mabaunsa wanaoishushia hadhi tasnia ya ubodigadi.


Pia amesema kuwa ameamua kuanzisha kampuni ambayo inashughulika na masuala ya ulinzi ili kuweza kulinda vigezo vya kiusalama ili kuweza kuondokana na mabaunsa wasio na vigezo.